Jumanne 27 Oktoba 2026 - 16:59
Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa Akutana na Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi/ Yasisitizwa Kutimizwe Masharti ya Iran kwa Lengo la Kumaliza Vita

Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei amelielezea Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na sekretarieti yake kuwa ni «makutano ya njia nne za usimamizi na mipango» ya masuala ya nchi. Aidha, amesisitiza kuhusu athari za pande zote kati ya nyanja nne za «utamaduni», «siasa», «uchumi» na «usalama», pamoja na umuhimu wa kuambatanisha maamuzi yanayochukuliwa katika kila nyanja na mipango inayolingana na nyanja husika.

Kwa mujibu wa SShirika la Habari la Hawza, Meja Jenerali Dkt. Muhsen Rezaei, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa, amekutana na Ayatullah Sayyid Mujtaba Khamenei, Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu.

Baraza Kuu la Usalama wa Taifa ni makutano ya njia nne za usimamizi wa masuala ya nchi

Katika mkutano huo, Ayatullah Sayyid Mujtaba Husseini Khamenei amelielezea Baraza Kuu la Usalama wa Taifa na sekretarieti yake kuwa ni «makutano ya njia nne za usimamizi na mipango» ya masuala ya nchi. Pia, amesisitiza kuhusu athari za pande zote kati ya nyanja nne za «utamaduni», «siasa», «uchumi» na «usalama», pamoja na umuhimu wa kuambatanisha maamuzi yanayochukuliwa katika kila nyanja na mipango inayolingana na nyanja husika.

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kuwa; kutumia ramani ya njia inayotegemea picha kamili ya kila hatua—kuanzia mwanzo hadi mwisho—ni sharti la msingi la kufanya maamuzi madhubuti na imara.

Miongoni mwa masuala mengine yaliyojadiliwa katika kikao hicho ni kuimarisha mshikamano na umoja wa kitaifa, pamoja na kuimarisha kuaminiana kati ya wananchi na viongozi; kutumia uwezo uliopo katika Katiba, hususan Ibara ya 176, ili kumsaidia Rais na vyombo vya utendaji kurahisisha na kuharakisha utatuzi wa matatizo ya nchi; kulinda usalama wa kitaifa na wa kikanda kwa kusimamia Mlango-Bahari wa Hormuz; na kuimarisha uhusiano wa pande mbili na nchi jirani kwa msingi wa maslahi ya kudumu na ya pande zote.

Kiongozi Mkuu wa Mapinduzi ya Kiislamu ameeleza kuwa; adui kufikia hali ya kukata tamaa ni miongoni mwa matunda ya muqawama na ustahimilivu wa kitaifa. Aidha, amesisitiza umuhimu wa kutoa taarifa kwa umakini na kwa wakati unaofaa ili kuhakikisha wananchi wanaendelea kujitokeza katika kuilinda nchi na mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu. Pia, amesisitiza kufuatilia upatikanaji wa haki na maslahi ya taifa la Iran na ya Muqawama kupitia kutimizwa masharti yaliyotangazwa na viongozi wa nchi, kwa lengo la kumaliza vita na hali ya «kutokuwa vitani wala kuwa na amani».

Katika kikao hicho, Katibu wa Baraza Kuu la Usalama wa Taifa aliwasilisha ripoti kuhusu hali ya nchi katika nyanja mbalimbali na juhudi zinazoendelea kufanyika.

Katika ripoti yake, Dkt. Muhsen Rezaei aliashiria kufuatilia sera ya kimkakati ya Jamhuri ya Kiislamu ya «kuweka utaratibu na kuanzisha mfumo wa kikanda unaojitegemea» kuwa miongoni mwa hatua ambazo sekretarieti ya Baraza Kuu la Usalama wa Taifa inaendelea kuzitekeleza.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha